Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo March 2, 2018 imewahukumu miaka 20 jela watu watatu akiwemo Mwanajeshi wa (JWTZ) EX MT.66807 SGT George Kwisema Senda baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kukutwa na vipande 10 vya meno ye Tembo vyenye thamani ya Shilingi Milioni 198.
Mbali na Mwanajeshi huyo, wengine waliohukumiwa ni Asha Ulaya na Nia Bakari ambapo pia mahakama hiyo imemuachia huru Shafii Muhibu.
Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mahira Kasonde baada ya wakili wa serikali Elia Athanas kuomba washtakiwa wapewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.
Hakimu Kasonde amesema mahakama hiyo imewatia hatiani washtakiwa watatu kati ya wanne kwa makosa ya kukutwa na nyara za serikali ambayo ni Meno ya Tembo baada ya kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka.
Katika kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi namba 22 ya mwaka 2016 Hakimu Kasonde amesema anawahukumu washtakiwa kwenda jela miaka 20 kwa kila kosa ambapo adhabu hiyo itaenda sambamba.
“Ninawahukumu kwenda jela miaka 20 kwa kila kosa na adhabu hiyo itaenda sambamba, pia namuachia huru mshtakiwa wa nne ambaye ni Shafii Muhibu kwa sababu hajatiwa hatiani,” -Hakimu
Washtakiwa walikabiliwa na kesi ya kukutwa na nyara za Serikali, ambapo inadaiwa June 2,2016 maeneo ya Mbagala Kibondemaji ambapo walikutwa na vipande 10 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya Sh.Mil 198,000,000.
Pia walikabiliwa na kosa la kujihusisha na biashara ya meno ya Tembo ambapo inadaiwa walitenda kosa hilo May 24,2016 na June 2,2016.
Inadaiwa katika maeneo ya Lindi na Dar es Salaam walikubaliana kusafirisha nyara hizo ambazo ni vpande 10 vya meno ya Tembo vikiwa na thamani ya Tsh.198,000,000.
BREAKING: Baadhi ya Viongozi wa ACT Wazalendo wahamia CCM