Duniani

Sahau majengo mazuri ya Dubai, sasa Falme za Kiarabu wana mpango wa kutengeneza mlima ili?

on

Falme za Kiarabu imeweka wazi mpango wake mradi mkubwa wa kujenga mlima lengo ikiwa ni kuongeza mvua, taifa hilo ambalo ni jangwa lina matumaini ya mradi huo mkubwa kuwa utasaidia kutengeneza mawingu ambayo yataleta mvua.

Wanasayansi kutoka Kituo cha Taifa cha Utafiti wa Anga ( NCAR ) kinachoendeshwa na US-based University Corporation for Atmospheric Research (UCAR)  kwa sasa wako katika awamu ya kwanza ya utafiti wa kina ili kuamua juu ya maeneo ya kujenga mlima huo na urefu na upana utakaohitajika.

Mtaalam wa mipango ya hali ya hewa ya muundo kutoka (NCAR), Roelof Bruintjes aliiambia Arabian Business kuwa………>>> “Kujenga mlima si jambo rahisi, bado tunamalizia kufanya mlinganisho wa maeneo hasa tukiangalia hali ya hewa”

>>>”Kama mradi utaonekana kuwa na gharama kubwa mno kwa serikali, mradi unaweza usiendelee lakini hii itawapa wazo au njia mbadala ya muda mrefu kwa ajili ya baadaye na Kama mradi utaendelea mpaka awamu ya pili tutakwenda kwenye kampuni ya uhandisi kuamua kama inawezekana au la

Source: http://www.independent.co.uk/news/world/middle-east/uae-build-mountain-fake-increase-rainfall-rain-man-made-cloud-seeding-a7013461.html

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

ULIIKOSA HII YA DIAMOND STUDIO ALIVYOREKODI ‘COLOURS OF AFRICA’ NA MAFIKIZOLO SOUTH AFRICA? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments