Waziri wa Fedha Tanzania Dr. Philiph Mpango amewaeleza Watanzania kila kilichosemwa kwenye mazungumzo IKULU na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia ambaye ameitembelea Tanzania ambapo moja ya vilivyojadiliwa ni Fly Over ya Ubungo ambayo itasaidia sana kuondoa foleni sugu.
- Kulikua na mazungumzo rasmi yaliyofanyika IKULU na kubwa la kwanza ilikua ni kuihakikishia benki ya Dunia kwamba kwa kweli ni wabia wetu wazuri wa maendeleo na Rais amesisitiza kwa upande wa serikali tutaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na benki ya dunia.
- Eneo moja ambalo Rais ameiomba Benki ya dunia itusaidie kuharakisha kuanza utekelezaji ni pale Ubungo kwenye makutano ya zile barabara.
- Huu mradi wa Mabasi yaendayo kazi hautakuwa na ufanisi kama bado pale Ubungo utategemea Askari wa barabarani kuongoza magari kwahiyo Rais Magufuli amesisitiza zaidi.
- Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia amekubali kwamba wataharakisha ule mchakato ili ujenzi wa barabara za juu kwenye makutano ya barabara Ubungo uanze.
- Kuhusu gharama za ujenzi wa Fly Over Ubungo hatuna namba kamili kwa sasa kwasababu bado tunakamilisha majadiliano lakini kwa takwimu za awali haitapungua Dola za Kimarekani MILIONI 60.
ULIPITWA? Tazama hapa chini ulipofikia ujenzi wa jengo jipya la kisasa ( Terminal 3 ) Aiport Dar es salaam