Ubalozi wa Marekani umesema kuna hatari kubwa ya mashambulizi ya Urusi kabla ya Siku ya Uhuru wa Ukraine siku ya Jumamosi.
Mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya Ukraine huenda yakaongezeka katika siku zijazo huku Kyiv ikijiandaa kuadhimisha miaka 33 tangu uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa Muungano wa Sovieti.
“Ubalozi wa Marekani mjini Kyiv unatathmini kwamba katika siku kadhaa zijazo na mwishoni mwa juma kuna ongezeko la hatari ya … ndege zisizo na rubani na mashambulizi ya makombora ya Urusi kote Ukraine kuhusiana na Siku ya Uhuru wa Ukraine mnamo Agosti 24,” ilisema.
Taarifa hiyo iliwekwa kwenye tovuti ya ubalozi huo usiku wa kuamkia jana.
Kwa Waukraine, Siku ya Uhuru imechukua umuhimu mkubwa tangu uvamizi wa Urusi, ambao umezua hisia za kizalendo miongoni mwa watu wengi.