Mahakama nchini Italia imeamuru mfanyakazi wa kampuni ya simu alipwe na kampuni hiyo baada ya kuridhika na ushahidi kuwa alipata uvimbe kwenye ubongo uliosababishwa na matumizi ya simu aliyopewa na kampuni hiyo.
April 21, 2017 mtandao maarufu wa Dail Mail ulichapisha stori kuwa Roberto Romeo alipewa simu na kampuni ya Telecom Italia ambayo alikuwa anaitumia saa tatu kwa siku kwa kipindi cha miaka 15 akiwa kazini ambapo kutokana na matumizi hayo aliota uvimbe kwenye ubongo na kupoteza uwezo wake wa kusikia katika sikio moja.
Mahakama katika mji wa Ivrea iliiamuru kampuni ya Telecom Italia ambayo ni maarufu kwa huduma za mawasiliano ya simu kumlipa Romeo hadi euro 7,000 ($7,500) ambazo ni zaidi ya Tsh. 16m kwa mwaka katika kipindi chote cha maisha yake baada ya madaktari kuthibitisha kuwa mwili wake umeathirika kwa 23% kutokana na matumizi ya simu.
Hii ni kesi ya kwanza duniani kuhukumiwa kwa kutambua uhusiano uliopo baina ya matumizi ya simu na kupata uvimbe kwenye ubongo ambapo muajiriwa huyo, alitumia simu ya kampuni kwa saa tatu kila siku kwa muda wa miaka 15 bila kuchukua tahadhari yoyote, hivyo kupelekea uvimbe kwenye ubongo na kupoteza uwezo wa kusikia kwa sikio moja.
Video: Fahamu kwa nini simu zinazuiliwa kwenye vituo vya mafuta. Bonyeza play kutaama.