FUNGUO, kwa kushirikiana na mpango wa iMBEJU chini ya benki yaCRDB, imezindua kundi la tatu linaojumuisha biasharachanga 18 na biashara bunifu ndogo na za kati, ikiwa nimafanikio mengine ya kuunga mkono shughuli za ujasiriamaliza Kitanzania.
Kutokana na mchakato wenye ushindani mkaliambao ulivutia maombi zaidi ya 400 nchi kote, kundi hililitanufaika na Shilingi Bilioni 1.45 katika mfumo wa RuzukuChocheo kutoka FUNGUO na Shilingi Milioni 355 kupitiaMikopo Nafuu ya iMBEJU.
Mpango huu unaonyeshakujizatiti kuimarisha biashara bunifu zilizojikita kuletamabadiliko yanayochangia kuzalisha ajira, kuwezesha vijana, na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania.
Ushirikiano huu wa kimkakati unaunganisha mageuzi, ruzukukutoka FUNGUO inayotolewa bila matarajio ya kurudishwa, ikiwa umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya pamoja na mikopoyenye masharti nafuu kutoka Taasisi ya Benki ya CRDB kupitia mradi wa iMBEJU, unaokuza fursa ya biashara changa kukua na kustawi. Ukizingatia, 40% ya fedha zilitengwa kwabiashara zinazoendeshwa na kuanzishwa na wanawake, kusisitiza umuhimu wa ujumuishwaji wa kijinsia katikakukuza mfumo bunifu na ukuaji wa Uchumi wa Tanzania.
Ikilenga kubadili hali ya Maisha kwa njia endelevu, biasharachanga zilizochaguliwa zinatoka sekta tofauti, ikiwemokilimo, nishati, Uchumi rejelefu, huduma za afya na kifedha, mara nyingi zinazotoa ufumbuzi unaotumia teknolojia. Biashara hizi zinalenga kushughulikia changamotozinazoikabili jamii wakati zikizalisha fursa za ajira, hususanikwa vijana. Mpaka sasa, wawekezaji wa FUNGUO kwapamoja wamekusanya Shilingi Bilioni 15.5 kama fedha za ziada na kuzalisha zaidi ya ajira 4,000 za moja kwa moja nazisizo za moja kwa moja, ambapo kundi la mwaka huulinatarajiwa kukuza zaidi mafanikio haya.
Zaidi ya ufadhili, biashara hizi changa zitapokea usaidizimaalum wa kiutaalamu, kuonyeshwa fursa, na kutengenezewawasifu wa uwekezaji ili kuongeza kasi ya ukuaji wao nakuvutia zaidi ufadhili.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Mheshimiwa Jerry Silaa, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia yaHabari, amesema,
“Ubunifu ni uti wa mgongo wa maendeleoya taifa letu, na leo, tukishuhudia uzinduaji wa kundi la tatu la wawekezaji chini ya Mpango wa FUNGUO Innovation kwakushirikiana na iMBEJU, tunasherehekea Mawazo thabiti naari ya kuhamasisha ujasiriamali kwa mustakabali waTanzania.
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia yaHabari imejizatiti kuunga mkono jitihada kama hizi ambazo zinawezesha biashara changa kutengeneza suluhisho kwa ajiliya manufaa ya jamii zetu na kuchangia Uchumi jumuishi nawa kidigitali.”
Balozi Christine Grau, Mkuu wa Ujumbe wa Umoja waUlaya, amebainisha manufaa mapana: “Umoja wa Ulayaunajivunia kuunga mkono biashara changa za Kitanzaniakupitia ufadhili chochevu, kuimarisha nafasi muhimu yaubunifu katika kukuza mabadiliko ya kiuchumi.
Kupitia zaidiya Shilingi Trilioni Moja ambayo imetengwa kwa ajili yamaendeleo ya sekta binafsi, tunakuza mfumo ambao wa jasiriamali wanaweza kustawi na kutengeneza ajiraendelevu kwa ajili ya vijana.”
Shigeki Komatsubara, Mwakilishi Mkazi wa UNDP, amesisitiza umuhimu wa kuwekeza kwenye vipaja vichanga, akibainisha, “Vijana wa Tanzania ni nguvu muhimu ya kuletamabadiliko. Kupitia miradi kama FUNGUO, tunawapatiafursa ya kuonyesha uwezo wao, kuwahakikishia wanakuwa narasilimali za kuvumbua, kukua, na kukuza mustakabali waUchumi wetu.”
“Ningependa kuonyesha namna gani tunavyojivunia kupitiawajasiriamali wa aina yake ambao wamechaguliwa. Ufadhilihuu ni zaidi ya msaada wa kifedha; ni fursa ya kubadilishabiashara zenu kuwa zenye manufaa yatakayodumu kwa mudamrefu. Utumieni ili kukua, kujifunza, na kushikilia kila fursaya kupata usaidizi wa kitaalamu na ushauri ambazoutaambatana nazo. Kwa pamoja, hatujengi biashara pekee – pia tunatengeneza ajira, kubadili Maisha, na kukuzamaendeleo endelevu ya jamii yetu.” – Joseph Manirakiza, Meneja Programu ya FUNGUO.
“Lengo letu ni kufungua milango ya fursa mbalimbali za ufadhili kwa biashara changa nyingi kwa kutumia fursa yakuchanga miundo tofauti ya ufadhili, tukichanganya ruzukuna mikopo yenye masharti nafuu ili kutoa msaada maalumkwa kila mmojawapo. Zaidi ya ufadhili, tumejizatiti kutoamsaada wa ushauri, kuwaunganisha na wadau waliopokwenye mfumo, na rasilimali ili kuhakikisha mafanikio yamuda mrefu ya biashara hizi changa. Hivyo, tungependa kuwana vijana wengi wenye uwezo kadri tuwezavyo,” amesisitizaBi. Tully.
Historia inayokua, tangu kuanzishwa kwake, FUNGUO imeonyesha nguvu ya uwekezaji wa kimkakati katika biasharachanga ili kutengeneza manufaa ya muda mrefu ya kijamii nakiuchumi. Kwa kushirikiana na taasisi zenye malengoyanayoendana kama vile mpango wa iMBEJU chini ya Benkiya CRDB, mpango unaoendelea kukuza wigo wake nakuimarisha mfumo wa biashara changa wa Tanzania.
Hatua hii ya mafanikio ni uthibitisho tosha wa nguvu yamabadaliko inayotokana na ushirikiano baina ya washirika wamaendeleo, taasisi za sekta binafsi, na serikali katikakuwawezesha wajasiriamali, kuzalisha ajira, na kuongeza kasi ya maendeleo kuelekea Malengo ya Maendeleo Endelevu(SDGs).