Isaya Mwakajana Lalika alizaliwa Kihesa, Mkoa wa Iringa, 02 January 1993 na Kabila lake ni Mhehe, Kijana Mbunifu wa Maudhui, Mpiga Picha Mahiri, Mhariri wa Makala na Mwandishi wa habari kutoka nchini Tanzania.
Mwakajana anafahamika sana kwa Ubunifu wa Maudhui, Upigaji picha Mnato na Jongefu katika Matamasha, Wanasiasa na Viongozi wakuu wa Nchi ya Tanzania; Isaya Mwakajana Alianza kutambulika zaidi baada ya Kampeni za Urais wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Kwa Ndugu Joseph Pombe Magufuli mwaka 2015 kabla ya Mwaka 26 April 2016 kujiunga na Clouds Media Group.
Pia Mwakajana amekuwa maarufu zaidi Afrika Mashariki kwa wepesi wake wa kutoa habari kwa haraka, matukio kama: siasa, michezo, burudani na Utalii mbali ameibua jina lake katika ulimwengu wa ubunifu hapa nchini Tanzania; Mwakajana ameonyesha uwezo wake mkubwa kwa kufanya kazi na watu mashuhuri kama wanasiasa, viongozi wa serikali, na kushiriki katika matamasha makubwa kama Fiesta na Malkia wa Nguvu.
Kazi yake katika uandaaji wa video imekuwa chachu ya mabadiliko, huku akileta sura mpya na ya kuvutia katika tasnia ya uandaaji maudhui nchini; Kupitia ujuzi wake wa kipekee, Mwakajana ameweza kubadilisha maisha yake na kuweka alama yake katika soko la ubunifu.
Moja ya mafanikio makubwa ya Mwakajana ni ushirikiano wake na watu mashuhuri, wanasiasa, na viongozi wa serikali, katika umri wake mdogo ameweza kuonyesha uwezo wa kipekee wa kubuni maudhui yanayogusa hisia na kuhamasisha watu mbalimbali hasa Kazi zake zimekuwa chombo cha kuwasiliana na jamii, ikileta taswira ya kipekee katika maisha ya watu maarufu, kijana huyu ashiriki katika Matamasha makubwa kama Fiesta 2017-2021, Malkia wa Nguvu, East Africa Got Talent (EAGT) Mashindano ya kusaka vipaji yaliyofanyika mwaka 2019 katika nchi nne za Afrika Mashariki akiwa mwongozaji na mpiga picha tegemeo katika Matukio haya makubwa ambapo Mwakajana ameshiriki kikamilifu kwa kuleta ubunifu, nguvu mpya na mtazamo wa kisasa katika matukio haya yaliyothibitisha kipaji chake katika tasnia ya burudani.