fB insta twitter

Magonjwa sita yanayosumbua Taifa yametajwa, matatu ya kuambukiza

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Moja ya habari zilizoandikwa kwenye magazeti ni hii kwenye gazeti la Jambo Leo yenye kichwa cha habari ‘Magonjwa Sita yatikisa nchi’

 

Gazeti la Jambo Leo limeripoti kuwa Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, wazee na watoto imetaja magonjwa makuu sita; kuwa ndiyo yanayolisumbua taifa kwa sasa. Magonjwa hayo ni matatu ya kuambukiza, ambayo kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Hamis Kigwangalla ni malaria, UKIMWI, kifua kikuu, kisukari, moyo na selimundu.

Kigwangalla aliyasema hayo katika mahojiano maalum na gazeti hilo na kusema magonjwa hayo ni hatari yanapaswa kuchukuliwa hatuaza haraka na dharura kuyadhibiti kwani ndiyo yanayoongoza kwa vifo vya watu wengi zaidi ikilinganishwa na mengine.

Unaweza kuzipitia hapa habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya Tanzania

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 10  KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments