Tukiwa bado tuko kwenye headlines za Uchaguzi 2015 stori inayochukua kasi katika vyombo vya habari pamoja na mitandao ni kuhusiana na wananchi kusimama mita 200 pale wanapomaliza kupiga kura siku ya tarehe 25, 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Tulia Ackson..’Mimi siamini kama uamuzi utakuwa umechelewa kwasababu kesi yenye imechelewa kuja kwa hiyo mimi ninaamini wananchi wafuata sheria watafuata taratibu watafuata yale waliyoelekezwa hata kwenye vituo vya kura au chochote kile watakachoelekezwa’ – Tulia Ackson
‘Kifungu cha 104 ibara ya ndogo ya kwanza kinayohistoria inayosema kwamba mtu haruhusiwa kufanya mkutano siku ya Uchaguzi kiliongezwa 1996 kwa hiyo kabla hakikuwepo kwasababu hakukuwa na haja ya hicho kifungu lakini kwa kuona kwamba kuna hilo hitaji hicho kifungu kikarekebishwa kikaongezewa hilo katazo la mtu kufanya mkutano kwa hiyo kile kifungu cha 104 ibara ya ndogo ya kwanza hakina utata wowote lakini wananchi wanataka kujua uhalisi ni upi ndio kilichotuleta mahakamani’ – Tulia Ackson
‘Mimi ninaona mjadala unaenda vizuri kwasababu upande wa mleta malalamiko amesikilizwa kwa kirefu mahakamani itapata fursa ya kupima hizi hoja za pande mbili itatoa uamuzi ambao unaona uko sawa kwa kile kifungu kinachobishaniwa na pia kwa mujibu wa katiba, kisheria anayepaswa kulinda kura ni polisi na kifungu cha 72 kimesema wazi’ – Tulia Ackson
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Naibu Mwanasheria Mkuu
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.