Michezo

Uchaguzi Simba: Godfrey Nyange Kaburu ampata mpinzani umakamu wa rais

on

Homa ya uchaguzi mkuu wa Simba inazidi kupanda, baada ya jana Evans Aveva na Micheal Wambura kuchukua fomu za kugombea uraisi wa klabu ya Simba SC, leo wanachama maarufu wa klabu hiyo Godfrey Nyange Kaburu na Joseph Itang’are maarufu kama Mzee Kinesi nao wamechukua fomu za kugombea umakamu wa raisi wa klabu hiyo.

Kaburu na Mzee Kinesi wote waliwahi kushika nafasi za juu kwenye uongozi uliopita wa Simba, lakini sasa wanaenda kwenye uchaguzi ujao wa Simba kuamua nani atakuwa makamu wa kwanza kabisa wa klabu hiyo.

Risiti ya malipo ya fomu za kugombea umakamu za Kaburu

Risiti ya malipo ya fomu za kugombea umakamu za Kaburu

 

SOURCCE: SHAFFIHDAUDA.COM

Tupia Comments