Rais wa sasa wa Madagascar Andrey Rajoelina anaongoza uchaguzi wa Alhamisi iliyopita, akiwa na asilimia 62.4 ya kura kwa sasa akifufuatwa na Siteny Randrianasoloniaiko kwa 12.2% na kumfukuza rais wa zamani Marc Ravalomanana kwa 11.2%.
Tume ya uchaguzi nchini humo ilisema waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 43 pekee huku baadhi ya wagombea wa upinzani wakihusisha ushiriki mdogo na wito wao wa kususia uchaguzi.
Wagombea 10 kati ya 12 wa upinzani walisusia kutokana na wasiwasi kuhusu uadilifu wa kura.
Mwezi Juni, Madagaska ilitikiswa na ufichuzi kuwa rais huyo alipata uraia wa Ufaransa mwaka 2014, jambo ambalo upinzani unadai kuwa linafaa kusababisha kupoteza uraia wake wa Madagaska na kumnyima sifa za kushiriki kinyang’anyiro hicho.
Rajoelina, ambaye anawania muhula wa tatu, anasema shutuma hizo ni mbinu ya kisiasa isiyo na msingi. Amesema kuwa katiba haimhitaji mkuu wa nchi kushikilia uraia wa Malagasy pekee, na kwamba serikali italazimika kuidhinisha kupoteza kwake utaifa.