Top Stories

Edward Lowassa mbele ya waandishi wa habari baada ya matokeo ya Uchaguzi

on

‘Leo  tarehe 29, October 2015  kupitia Mgombea mwenza Mh, Juma Duni Haji aliwasilisha rasmi  malalamiko kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi mkuu wa 2015 kwa mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ‘ – Edward Lowassa

‘Tumeainisha kwenye malalamiko yetu kutokuridhisha kwetu na mwenendo na matukio mbalimbali hususani, utangazaji wa matokeo batili, yasiyo akisi matokeo halisi yaliyopatikana katika vituo vya kupigia kura kama ifuatavyo’ – Edward Lowassa

1.Upunguzwaji wa kura zangu

2.Kuongeza kura kwa wagombea wa CCM

3.Kuendelea kukataa dhuluma hii dhidi ya matakwa ya wananchi, na jaribio la kutaka kubakwa kwa demokrasia kunaonekana wazi kutokana na mwenendo wa tume kuendelea kutangaza matokeo yasiyo ya kweli kupora ushindi wetu

Aidha kumekuwepo pia na uporaji kwa wagombea Wa vyama vya Ukawa kwenye ngazi ya Ubunge na Udiwani.

.

.

‘Kama tulivyoeleza jana takwimu zetu sisi zilionesha kwamba nilikuwa naongoza kwa zaidi ya 67% na sasa tumejiridhisha kwamba nimepata kura 10, 268, 795 sawa na asilimia 62% baada ya kukamilisha kazi ya kukusanya fomu za matokeo nchi nzima  kwa hali hii, ninaitaka tume ya taifa ya Uchaguzi itangaze mara moja mimi Edward Ngoyai Lowassa kuwa mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’ – Edward Lowassa

‘Tanzania kwa miaka mingi imefahamika kama kisiwa cha Amani katika Afrika, tunashangaa leo kuona vyombo vya ulinzi na Usalama vikitanda kila mahali wakiwa na silaha za kivita mitaani kana kwamba uchaguzi ni vita hii ni kuwatisha wananchi  ili wakubali kunyang’anywa haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanao wataka, nina amini watanzania hatutakubali hali hiyo’ – Edward Lowassa.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTERFB YOUTUBE.

Tupia Comments