Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri yaWilaya ya Kasulu, Dkt. Semistatus H. Mashimba ametoa maelekezo ya Uchaguzi waSerikali za Mitaa wilayani humo kwa kutumiamfumo unaoakisi 4R za Mhe. Rais Dkt. SamiaSuluhu Hassan kwa kushirikisha makunditofauti katika jamii.
Tukio hilo limefanyika leo Alhamisi Septemba26, 2024 katika Ofisi za Makao Makuu yaHalmashauri hiyo eneo la Nyamnyusi nakuhusisha viongozi wa vyama vyasiasa,viongozi wa dini,wazee maarufu,vyamavya wafugaji na wakulima,watendaji wa vijiji nakata pamoja na waandishi wa habari.
Akizungumza katika tukio hilo Dkt. Mashimbaamesema kuwa ni takwa la kisheria lililomtakakufanya hivyo ili wananchi wapate maelezosiku 62 kabla ya tarehe ya uchaguzi kwa lengola kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa kwawapiga kura pamoja na wagombea kupatataarifa zote kwa wakati.
“kampeni zitaanza tarehe 20 hadi 26 Novemba2024 na uchaguzi utakuwa Novemba 27 mwakahuu kwahiyo tuwaombe vyama vyasiasa,viongozi wa dini na wadau wote mliopohapa tunaomba kipindi hiki kiwe na utulivu naamani kubwa tofauti na mazingira mengine,” amesema.
Naye Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kasulu, Abdallah Kazikwa ametoawito kwa wananchi kujitokeza kwa wingikujiandikisha katika Daftari la Mkazi ambalo nitofauti na zoezi lililopita la uandikishwaji katikaDaftari la Kudumu la Mpiga Kura ili wawezekuitumia haki yao ya msingi ya kuchaguaviongozi wanaowafaa.
Kwa upande wao viongozi wa vyama rafikiWilaya ya Kasulu wameipongeza Kamati yaUchaguzi kwa kuwashirikisha katika tukio hilomuhimu huku wakibainisha kuwa na imaninayo pamojana kutoa ahadi kuipa ushirikianopale uatakapohitajika.
Katika hatua nyingine Katibu wa Baraza la Machifu Mkoa wa Kigoma,Abel Bussa ametoarai kwa kila mwananchi mwenye sifa kujitokezakugombea pamoja na kutoa ahadi ya kwendakufundisha aliyojifunza leo kwa wengine juu yaumuhimu wa kupiga kura.