NI Mkali kutokea Bongo Flevani, Nasseb Abdul a.k.a Diamond Platnumz ambae July 29, 2021 ametuletea video mpya ya wimbo wake uitwao IYO aliyowashirikisha wakali kutoka Afrika Kusini akiwemo Focalistic, Mapara A Jazz & Ntosh Gazi.
Kupitia Collabo hii aliyoifanya Diamond inakwenda kumuweka katika charts mbalimbali nchini Afrika Kusini hususani kwenye muziki wao wa sasa unaotamba unaofahamika kama Amapiano.
Najua nina watu wangu ambao mtakuwa mnajiuliza kwanini Diamond Platnumz aliamua kuwashirikisha wasanii hawa wa Afrika Kusini kwenye wimbo wake mpya uitwao IYO akiwemo Focalistic, Mapara A Jazz & Ntosh Gazi.
1.FOCALISTIC
Tukianza na Focalistic ni msanii kutoka Afrika Kusini ambae Afrika imemtambua baada ya kuachia wimbo wake uliotamba katika charts mbalimbali uitwao KE STAR.
PITORI MARADONA a.k.a Focalistic akihojiwa kwenye kituo kimoja cha Radio anakiri na kusema KE STAR ndio wimbo bora kwake uliomuweka kwenye ramani ya muziki wa Afrika na kuweza kupata mafanikio.
Video ya wimbo huo mpaka sasa kupitia mtandao wa Youtube umetazamwa na wafuasi Milioni 6,535,899 huku akiwa tayari ameshapata shows mbalimbali kutoka Afrika zikiwemo Tanzania, Kenya, Ghana, Nigeria na nyinginezo.
Mbali na KE STAR kuingia katika charts mbalimbali staa huyo mwaka 2020 aliamua kuachia rasmi album yake aliyoipa jina la Sghubu Ses Excellent ambayo ina nyimbo zaidi ya 10
1. Focalistic – Sghubu Ses Excellent (feat. Madumane, MDU aka TRP, Bongza
2. Focalistic – Ke Star (feat. Vigro Deep)
3. Focalistic – Tashkuma (feat. Mellow & Sleazy, Tyler ICU)
4. Focalistic – Onoroko (feat. Riky Rick, Semi Tee, Reece Madlisa)
5. Focalistic – Benz and Beamer (feat. Mas MusiQ)
6. Focalistic – Vrr Phaa (feat. Vigro Deep)
7. Focalistic – In Your Mind (feat. DJ Venom, DJ Maphorisa, Tyler ICU)
8. Focalistic – Stlamatlama (feat. 25k, Abidoza, Junior Taurus)
9. Focalistic – Billion
10. Focalistic – Palama (feat. DBN Gogo, Mellow & Sleazy)
11. Focalistic – Phalafala (feat. Mr JazziQ)
12. Focalistic – Blecke (feat. JazziDisciples)
13. Focalistic – Sefela (feat. Mas Musiq)
14. Focalistic – City on Fire (feat. Abidoza, Squad Sa Maradona)
Baada kuachia album yake aliyoipa jina la Sghubu Ses Excellent ndipo collabo zikaanza kumiminika yaani Nation to Nation, City to City, unaambiwa KE STAR ilimfungulia Dunia na kumpa collabo na msanii wa Nigeria, Davido ambapo Mnamo Febuari 2021 wawili hao waliiachia remix ya KE STAR.
Focalistic anaingia kwenye orodha ya wasanii wanaotokea katika bara la Afrika ambae ana mashabiki wengi pia aliepata mafanikio kwa haraka baada ya nyimbo zake kadhaa kuingia katika charts mbalimbali zikiwemo TV & Radio.
2.MAPARA A JAZZ
Mapara A Jazz ni kundi la muziki kutoka Afrika Kusini wakali hawa ni miongoni walioshirikishwa katika wimbo wa Diamond ‘IYO’.Mapara A Jazz umaarufu wao umeitikisa Afrika baada ya kuachia wimbo wao uitwao John Vuli Gate ambapo kupitia single hiyo wamepata Airtime kubwa kwenye charts za Radio hata TV.
3.Ntosh Gazi
Ntosh Gazi ni mkali kutoka Afrika Kusini ambae nae amesikika kwenye IYO ya Diamond Platnumz. Staa huyo Afrika inamtambua baada ya kushirikishwa kwenye wimbo uitwao John Vuli Gate ya wakali Mapara A Jazz ambayo mpaka sasa kupitia mtandao wa Youtube umetazamwa na zaidi ya watu duniani Milioni 8,802,347
4.TXC
TXC ni kundi la Ma Dj’z linaloundwa na warembo wawili akiwemo Tarryn & Clair Good news ambao ninataka kukusogezea ni kwamba warembo wao ni miongoni pia walioonekana kwenye video mpya ya IYO ya Diamond.Hii inatudhihirishia jinsi gani Diamond anavyotaka kuliteka vizuri soko la muziki wao unaotamba kwasasa.
Unaweza ukatazama hapa mbwembwe za TXC
5.Uncle vinny
Uncle Vinny ni msanii na mnenguaji ambae umaarufu ameupata baada ya kuwa ubunifu wa kucheza style tofauti za nyimbo zao zinazofahamika kama Amapiano.
Vinny amepata umaarufu wa ghafla baada ya kuonekana mara kwa mara kwenye Session iitwayo Balcon Mix Africa ya wakali Major League DJ’z akionesha mbwembwe za uchezwaji wa nyimbo zao.
Sasa leo baada ya video mpya ya Diamond Platnumz iitwayo IYO kuachiwa hewani nae amekuwa ni miongoni mwa watu walioonekana katika video hiyo mpya.
Hapa nimekusogeza ushuhudia baada ya matukio yake ya uchezaji yaliyompa umaarufu Afrika kupitia muziki wao uitwao AMAPIANO.
https://www.youtube.com/watch?v=hdbprd7Vli4