Takribani Safari za Ndege 4,500 zimcheleweshwa na nyingine 2,000 kuhairishwa huko Nchini Marekani kufuatia dhoruba kali ya majira ya baridi.
Baadhi ya picha kutoka katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Muhammad Ali wa Louisville huko Kentucky zinaonyesha ndege zikiwa zimefunikwa ma theluji.
Siku nzima tumekuwa tukifuatilia jinsi dhoruba hii ya msimu wa baridi inavyoathiri usafiri, huku viwanja vya ndege vikiwa na usumbufu mwingi.
Zaidi ya safari 5,000 za ndege ndani, ndani au nje ya Marekani zimechelewa kufikia sasa, kulingana na tovuti inayofuatilia FlightAware.
Katika baadhi ya maeneo ya Marekani ambapo theluji imekuwa ikianguka, maafisa wanajiandaa kwa hali kuwa mbaya zaidi.
Kufikia sasa, shule zingine zilikuwa zimeanza kughairi masomo ya Jumatatu.
Huko Kentucky, Indiana, Maryland, Washington, DC na Virginia shule tayari zimetangaza kufungwa.