fB insta twitter

Maumivu 18% miamala ya benki, wachumi waonya haya

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Moja ya stori iliyoripotiwa ni hii kwenye gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Maumivu 18% miamala benki ’

Baada ya taribani benki zote nchini kutangaza ongezeko la asilimia 18 kwenye huduma za kuhifadhi na kutoa fedha, kupitia gazeti la Nipashe wachumi mbalimbali walisema jana kuwa mbali na wafanyakazi ambao wataathirika na ongezeko hilo kwa sababu ya mishahara yao inapitia benki wamo wafanyabiashara na wanafunzi.

Gazeti hilo limeripoti kuwa wafanyabiashara, wanafunzi na wengine wote wanaotumia huduma za kibenki wataumia pia kwa kukatwa fedha zaidi wanapofanya miamala ya kibenki, walisema hali hiyo inaweza kufanya watu waamue kukaa na fedha majumbani mwao kitendo ambacho kitaongeza matukio ya uhaifu kwa majambazi kuvamia majumabani.

Gazeti hilo limesema kuwa Ongezeko hilo limetokana na marekebisho ya sheria ya kodi ya ongezeko ya thamani ‘VAT’, SURA 148, yaliyotangazwa na Waziri wa fedha na mipango, Dk Philip Mpango alipokuwa akisoma bajeti ya Serikali  kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Mpango alisema Serikali inakusudia kutoza kodi ya ongezeko la thamani kwenye ada za huduma za kibenki zinazotozwa na benki zote nchini ili kupanua wigo wa kodi. 

Unaweza kuzipitia hapa habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya leo julai mosi

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 01 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments