“Pamoja na changamoto mbalimbali zilizoikumba Dunia ikiwemo mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu, uchumi wa Tanzania umeendelea kuwa imara, kuendelea kukua kwa uchumi kumetokana na utekelezaji wa sera za bajeti na fedha chini ya uongozi thabiti wa Jemedari wetu JPM”- Waziri wa Fedha na Mipango, Dr.Philip Mpango leo Dodoma
“Katika kipindi cha January hadi September, 2020, Pato la Taifa lilikua kwa 4.7%, aidha mfumuko wa bei ulifikia wastani wa 3.5% January 2021 ikilinganishwa na 3.7% January 2020” – Waziri Mpango
“Riba za amana kwa kipindi cha mwaka mmoja zilipungua kufikia 8.41% December 2020 kutoka 8.90% December 2019 na riba za mikopo ya kipindi cha mwaka mmoja imepungua na kufikia wastani wa 15.72% December 2020 kutoka 16.28% December 2019”-MPANGO
“Thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani na sarafu nyingine Duniani imeendelea kuwa tulivu kutokana na utekelezaji wa sera thabiti za fedha na bajeti pamoja na kupungua kwa nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamisho wa mali nje ya Nchi”-MPANGO