Polisi wa Korea Kusini wanawachunguza wanajeshi 17 wa Marekani na watu wengine watano wanaodaiwa kusafirisha au kutumia bangi kupitia barua za kijeshi.
Hii inafuatia uvamizi katika kambi mbili za jeshi la Marekani mwezi Mei, ikiwa ni pamoja na Camp Humphreys, kambi yake kubwa zaidi ya ng’ambo.
Mfilipino na Mkorea Kusini wamekamatwa, huku waendesha mashtaka wakipitia kesi dhidi ya washukiwa wote 22.
Kidokezo kutoka kwa kitengo cha utekelezaji cha Jeshi la Marekani kilikuwa kimesababisha uchunguzi wa miezi minne na mamlaka ya Korea.
Ilikuwa ni moja ya kubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni iliyohusisha askari wa Marekani, vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kumnukuu Cha Min-seok, afisa mkuu wa upelelezi nchini Korea Kusini.
Uvamizi wa pamoja wa polisi wa Korea Kusini na Kitengo cha Upelelezi wa Jinai cha Jeshi la Marekani uligundua gramu 77 ya bangi , aidi ya kilo nne za “miminiko iliyochanganywa” inayotumika kwa kuvuta mvuke na jumla ya dola 12,850 pesa taslimu nyumbani kwa washukiwa 22′.
Saba kati yao wakiwemo askari watano wanadaiwa kuhusika na uuzaji wa dawa hizo, watumiaji 12 na watatu walikuwa wafanyabiashara wa kati.
Wanajeshi hao 17 kwa sasa wako katika kambi ya Humphreys, yapata kilomita 48 kusini mwa mji mkuu Seoul, na katika Camp Casey, kituo cha jeshi kilicho karibu kilomita 40 kaskazini mwa Seoul, kulingana na polisi.