Michezo

UCL: Alichowafanya Sergio Aguero Bayern Munich hiki hapa

on

IMG_9102.PNG

Japo ni vigumu kuamini, lakini ukweli ni kwamba mabingwa wa England – matajiri Manchester City bado wapo kwenye michuano ya ulaya pamoja na kuwa na pointi 5 kutoka kwenye kundi lao.

Jana wakicheza kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Etihad Manchester City wamepata ushindi wa kwanza kwenye michuano hii baada ya kuifunga Bayern 3-2.

‪Bayern Munich ndio walianza kufungwa kupitia goli la penati la Sergio Kun Aguero, lakini mpaka kufikia mapumziko Bayern walikuwa mbele kwa magoli ya Robert Lewandoski na Xabi Alonso.

Wakati wakiwa wameshapoteza matumaini ya kusonga mbele dakika ya 85 na 90 – Aguero tena akaifungia City magoli mawili na kuipa timu yake ushindi ambao umewapa pointi 5 sawa na Roma na CSKA Moscow.

Man City mchezo ujao wanacheza na Roma jijini Rome Italia – watahitaji kushinda huku wakiomba Bayern nae amfunge Moscow ili wapite kwenda hatua inayofuatia ya UCL.

Tupia Comments