Michezo

Ya Man City vs Bayern Munich ilikupita jana? matokeo ninayo hapa

on

IMG_7315.JPG

Ligi ya mabingwa Ulaya imeendelea tena September 17 2014 kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali barani Ulaya ambapo kule Etihad stadium Manchester waliikaribisha FC Bayern Munich kwenye mechi ya kundi E.

Mchezo huo uliowakutanisha mabingwa wa ligi za Ujerumani na England ulikuwa mgumu na mpaka kufikia dakika ya 90 bado matokeo yalikuwa 0-0, sifa zimuendee Joe Hart wa City kwa umahiri wa kuokoa michomo ya washambuliaji wa Bayern.

Katika dakika 3 za mwisho za nyongeza mchezaji wa zamani wa Man City -Jerome Boateng aliiadhibu timu yake ya zamani kwa kuifungia Bayern goli pekee na la ushindi kwenye mchezo huo.

Boateng alifumua shuti kali ambalo Hart alijaribu kulifata lakini likamshinda na kuipa Bayern ushindi ambapo kama ulimis mechi nimekupangia hapa pia jinsi timu zilivyopangwa:

Bayern Munich: Neuer 7, Rafinha 6.5 (Pizarro. 84), Boateng 7, Benatia 6.5 (Dante, 85), Bernat 7.5, Lahm 6.5, Alonso 6.5, Alaba 7, Muller 6.5 (Robben, 76, 5.5), Lewandowski 6.5, Gotze 7
Subs: Reina, Dante, Shaqiri, Pizarro, Rode, Hojbjerg.
Scorer: Boateng, 89.
Manager: Pep Guardiola, 6.5
Man City: Hart 9, Sagna 6.5, Kompany 7, Demichelis 6.5, Clichy 6, Nasri 5.5 (Milner, 58, 6) Fernandinho 6, Toure 5.5, Navas 6 (Kolarov, 87), Silva 7.5, Dzeko 6 (Aguero, 74, 5.5)
Subs: Caballero, Kolarov, Aguero, Lampard, Mangala, Boyata.
Manager: Pellegrini, 6.5

Unataka kuwa karibu na millardayo? unataka kutumiwa stori? jiunge na mimi kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>> twitter Insta FB

Tupia Comments