Mix

VIDEO: UDART wametaja njia walizozitumia kudhibiti ajali za mabasi yaendayo haraka

on

Wakati mabasi yaendayo haraka yalipoanza kutumika kulikuwa na mfululizo wa ajali ambazo ziliripotiwa zikihusisha mabasi hayo, June 8 2106 mbunge wa viti maalum CCM Amina Mollel aliliambia bunge kuwa mpaka mwezi june idadi ya mabasi yaliyopata ajali yalikuwa zaidi ya 30, na akaeleza kuwa gharama za matengenezo zilikuwa ni zaidi ya milioni 90.

Takribani miezi miwili iliyopita mabasi yaendayo haraka hayajaripotiwa kupata ajali ikilinganishwa na hapo awali, Ripota wa millardayo.com na Ayo TV amezungumza na afisa uhusiano wa UDART, Deus Bugaywa kutaka kujua njia walizozitumia kudhibiti ajali…..

>>>’Mwanzoni tulikuwa tuna rekodi ya ajali nyingi kwa sababu barabara zilikaa muda mrefu hazitumiki watu wakazizoea, elimu tunaendelea kutoa…………wananchi wameanza kuelewa kwa nini wanatakiwa waziache barabara hizo’

>>>‘Sasa hivi katika kituo chetu cha Jangwani tumejenga control room, unaweza ukawamonitor madereva unawaona kwenye screen, unaona gari gani limewahi, gari gani limechelewa, gari gani linaenda spidi’:Deus Bugaywa

ULIKOSA HII TAARIFA YA TETEMEKO LA ARDHI LILILOTOKEA BUKOBA LEO SEPT 10 2016? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

 

Soma na hizi

Tupia Comments