Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kupitia Shule Kuu ya Biashara waanzisha programu ya kufundisha mtaala wa kilimo ili kusaidia vijana kuweza kujiajiri na kuajiri wengine.
Akizungumza na wakati wa uzinduzi wa programu hiyo, Kaimu Mkuu wa shule ya Biashara (UDSM) Dkt Latifa Mbelwa amesema kuwa tumeanzisha programu hii ya kilimo cha biashara ili kusaidia wanafunzi kujiajiri.
Amesema tunataka programu zetu za shule kuu ya biashara ziendane na soko na mahitaji ya nchi ni makubwa sana kwenye sekta ya kilimo.
“Sekta ya kilimo inamchango mkubwa kwenye mapato ya nchi inaajiri vijana wengi kwa kiasi kikubwa na jamii ya watanzania, ni sekta inayowabeba wengi.”
“Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tunaona hii fursa ni muhimu kwenye mradi huu unataka tuwe na kozi ambazo mitaala inafanania na kuongeza uwezo na ujuzi, katika eneo la kilimo Biashara.” amesema Dkt Mbelwa
“Tupo kwenye kupitia programu zetu ni kipindi cha kuingiza ujuzi muhimu kwenye mitaala hii baada ya miaka kadhaa tutaweza kutoa wataalamu wazuri wa Biashara kwenye maeneo ya uhasibu wa masoko, banki kwenye ujuzi wa kilimo biashara.”
Naye Mkurugenzi wa (SUGECO) kampuni ya kusaidia vijana kujiajiri kupitia kilimo kutoka Chuo Kikuu cha sokoine, Revocatus Kimario, amesema wamejikita kufanya kazi na vijana waweze kujiajiri kupitia sekta ya kilimo kwa kubadiri fikra na mitazamo yao wakiona kilimo waone ni fursa ya biashara.
“Kuna programu tunashirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufundisha ujasiliyamali kwenye sekta ya kilimo inayolenga kuwaongezea vijana ujuzi na maarifa ya kutenda na kuwekeza kwenye kilimo kama fursa itakayowasaidia wao kujiajiri na kutengeneza fursa za kuajiri wengine.”