Top Stories

“Kila baada ya dk 10 msichana hufa duniani kutokana na ukatili” – Umoja wa Mataifa

on

Leo October 11, 2017 dunia yote ikiwa inaadhimisha siku ya mtoto wa kike, imeelezwa kuwa kuna wasichana bilioni 1.1 ulimwenguni mwote na wote hawa wana haki ya kupata fursa na haki sawa katika maeneo yote ya maisha.

Ripoti illiyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women limeeleza kuwa kila baada ya dakika 10 msichana mmoja aliyevunja ungo katika maeneo tofauti tofauti duniani hupoteza maisha kwa sababu zinazotokana na ukatili wa kijinsia.

Imeelezwa pia kuwa wasichana kwenye umri huu huwa kwenye hatari kubwa ya kuwa wahanga wa ukatili wa kingono, ndoa za utotoni, unyanyasaji na biashara haramu ya kusafirisha binadamu. UN Women imetoa wito kwa familia, wanajamii, wanaharakati na serikali kuhakikisha inawalinda watoto wa kike pamoja na maisha yao ya mbeleni.

Ulipitwa na hii? “Asilimia 12 ya vifo vyote nchini hutokana na saratani ya matiti” – Wizara ya Afya

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments