Ad
Ad

Michezo

Hat-trick ya Giroud yaipeleka Arsenal 16 bora, Cheki matokeo ya mechi za UEFA Dec 9 na list ya 16 bora (+Pichaz&Video)

on

Michezo ya kuhitimisha hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya imeendelea tena usiku wa December 9 kwa kupigwa mechi nane baada ya usiku wa December 8 kupigwa michezo nane ya Kundi A, B, C na D ila December 9 imechezwa michezo nane ya Kundi E, F, G na H, michezo hiyo ilichezwa wakati timu 10 kati ya 32 zikiwa zimeshajihakikishia nafasi ya kwenda hatua ya 16 bora hivyo nafasi 6 pekee ndio zilikuwa zinawaniwa.

3371

Klabu ya Arsenal ambayo ilikuwa nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi F, nafasi yake ya kuendelea hatua ya 16 bora ilikuwa mikononi mwake yenyewe, kwani ilitakiwa kuifunga Olympiakos ya Ugiriki kwa idadi nzuri ya magoli ili iweze kufuzu hatua ya 16 kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, kwani Olympiakos walikuwa wanahitaji suluhu tu ili wafuzu. Hata hivyo Arsenal ilifanikiwa kufuzu baada ya kuifunga Olympiakos kwa jumla ya goli 3-0.

2200

Arsenal ikiwa katika uwanja wa Stadio Georgios Karaiskaki ilipata magoli yake matatu yote kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga katika klabu hiyo Oliver Giroud, staa huyo aliyeipeleka Arsenal hatua ya 16 bora alianza kufunga goli la kwanza dakika ya 29, kipindi cha pili akamalizia kwa kupachika magoli mawili dakika ya 49 na dakika ya 67 kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Olympiakos kushika mpira katika eneo la 18.

3089

Hii ndio list ya timu zilizofuzu hatua ya 16: Real Madrid, PSGVfL WolfsburgPSV Eindhoven, Atletico Madrid, Benfica, Man City, Juventus, FC Barcelona, Roma, FC Bayern Munich, Arsenal, ChelseaDynamo KievZenit St P na KAA Gent.

Matokeo ya mechi nyingine za UEFA za December 9

Kundi E

  • Bayer Leverkusen 1 – 1 FC Barcelona
  • Roma 0 – 0 BATE Borisov

Kundi F

Kundi G

Kundi H

Video za magoli ya Olympiacos Vs Arsenal

https://youtu.be/BgmQNAWTUio

Video za magoli ya Bayer Leverkusen Vs FC Barcelona

https://youtu.be/qQig1WgIf7c

Video ya magoli ya Chelsea Vs FC Porto

https://youtu.be/wCTkcFUNJOA

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments