Michezo

Huu ni mpira maalum utakaotumika katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya 2015/2016 (Pichaz)

on

Kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Uingereza na Ligi Kuu Hispania mashirikisho ya soka ya nchi husika huwa wanatangaza aina ya mpira utakaotumika katika msimu husika, tayari tumeshaona mpira unaotumika katika Ligi mbalimbali barani Ulaya.

News-Picture-UEFA

August 26 umetangazwa mpira utakaotumika katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya msimu huu, licha ya kuwa ulitumika katika mechi ya kwanza ya mchujo katika ya Manchester United dhidi ya Bruges lakini August 27 ni siku ambayo utazinduliwa rasmi mpira huo katika mji wa Marseille Ufaransa.

Uzinduzi huo utapambwa na uwepo wa wachezaji wa vilabu vya Man United, Real Madrid, AC Milan, Bayern Munich, Chelsea na Juventus lakini ni siku ambayo droo ya makundi ya klabu Bingwa Ulaya itachezeshwa.

Hizi ni picha za mpira huo

Adidas-Finale-15-Champions-League-Official-Match-Ball (2)

Adidas-Finale-15-Champions-League-Official-Match-Ball

Adidas-Finale-15-Champions-League-Official-Match-Ball (1)

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

 

 

Tupia Comments