Michezo

Jose Mourinho na Iker Casillas kukutana tena, haya ndio yalioandikwa mitandaoni…

on

Ligi ya Mabingwa barani Ulaya inatarajiwa kuendelea siku ya Jumanne ya September 29 kwa vilabu kadhaa kushuka dimbani kupambana kusaka point tatu muhimu ili kuweza kujiongezea point na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya 16 bora licha ya kuwa bado mapema kujua timu gani itafanya vizuri.

Stori kutoka katika mitandao mbalimbali ya michezo duniani inazungumzia mchezo kati ya FC Porto ya Ureno dhidi ya Chelsea ya Uingereza, kikubwa ni kocha wa zamani wa klabu ya Real Madrid ya Hispania ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Chelsea Jose Mourinho atakapokutana na golikipa wake wa zamani wa Real Madrid Iker Casillas.

2CDAAE9600000578-0-image-a-11_1443433316632

Inadaiwa kuwa Jose Mourinho ni moja kati ya watu waliochangia Iker Casillas kushuka uwezo kutokana na maneno ya kocha huyo, ambaye mwaka 2010 wakati anajiunga na Real Madrid Iker Casillas ndio alikuwa ametoka kutwaa Kombe la Dunia, hivyo alikuwa na uwezo mzuri. Kinachovutia wengi ni kuwa September 29 wanakutana katika uwanja wa Estadio do Dragao mahali ambapo ulizaliwa ufalme wa “Special One”.

2CDAAE5A00000578-0-image-m-16_1443433393283

Lakini uwanja huo ndio uwanja wa nyumbani wa klabu ya FC Porto klabu ambayo anaichezea golikipa wa zamani wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania Iker Casillas. Hivi ni nani atashangiliwa? nani atazomewa? vipi kama Casillas akiyaona mabango yanayompokea Mourinho kwa heshima kubwa kuliko yeye itamuumiza? Jibu ni kesho mtu wangu wa nguvu.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata,pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE

Tupia Comments