Michezo

Full Time ya mechi za UEFA Feb 17 ikiwemo ya Roma vs Real Madrid

on

Usiku wa February 17 mechi za Gent dhidi ya Wolfsburg na mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya AS Roma ya Italia, ulikamilisha idadi ya timu 8 za kwanza kucheza mechi zake za kwanza za hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mchezo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu usiku wa February 17 wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ni mchezo kati ya Roma dhidi ya Real Madrid.

2925

Mchezo huo umemalizika kwa Real Madrid ya Hispania kuibuka na ushindi wa goli 2-0, licha ya AS Roma kuwa katika dimba lao la nyumbani, lakini hiyo haikuwa na manufaa kwao, kwani walikuwa wakimiliki mpira kwa asilimia 40 wakati Real Madrid walikuwa wanaongoza kwa asilimia 60.

3600

Goli la kwanza la Real Madrid lilifungwa dakika ya 57 na mchezaji bora wa dunia mara tatu Cristiano Ronaldo na Jesse Rodriguez alipachika goli la pili dakika ya 86, hivyo AS Roma watakuwa na wakati mgumu wa kwenda kubadili na matokeo katika mchezo wa marudiano Santiago Bernabeu ili watinge hatua ya robo fainali.

Matokeo ya mechi nyingine za UEFA February 17

  • Gent 2 – 3 Wolfsburg

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments