Michezo

Yasikupite ya Mechi za UEFA jana.. Real Madrid VS Atletico Madrid, Juventus VS Monaco

on

UEFA

Pazia la robo fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa Ulaya limefunguliwa leo ambapo Real Madrid imekutana na mahasimu wao Atletico Madrid kwenye uwanja wa Vicente Caldero, Spain.

Ronaldo

Haikuwa siku nzuri kwa staa Cristiano Ronaldo, hapa Koke na Mario Suarez walimuwekea ukuta wa nguvu.

Macho na masikio ya mashabiki yalikuwa upande wa mechi hii.. dakika 90 za mchezo zikakamilika kwa sare ya kutokufungana, 0-0.

Beki wa Real Madrid, Marcelo kabla ya mechi hiyo aliwaomba mashabiki wasiwe na hofu kwa kuwa kikosi chao kilikuwa kiko sawa kabisa, lakini imeonekana wapinzani wao pia walijipanga kuhakikisha hawafanyi makosa kuipoteza mechi hiyo ngumu.

Upande mwingine ilikuwa patashika kati ya vigogo wa Juventus na Monaco, dakika 90 zikakamilika pamoja na za nyongeza nyingine nne lakini Juventus walitoka kifua mbele kwa goli 1-0, ambapo Arturo Vidal alishinda goli hilo pekee kwa njia ya penalty.

Monaco

Arturo Vidal akikamilisha ushindi wa timu yake kwa penalty.

Kimbembe kingine kiko leo uwanjani, Bayern Munich watakunjana na FC Porto huku Paris SG wakishikana mashati na FC Barcelona.

millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments