Kutokana na kuwepo na vituo holela vya uegeshaji magari makubwa ya Mizigo katika eneo la Mikumi(Kidoma na Green) Wilaya ya Kilosa barabara ya Iringa – Morogoro kumetajwa kusababisha ongezeko la biashara haramu ya ngono ,ajali na uhalifu katika eneo hilo.
Wakizungunza na Kituo hiki wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa Morogoro Adam Malima, ambapo baadhi ya wakazi hao wanasema licha ya kuongezeka kwa Fursa za biashara kwa wajasiriamali hasa mama lishe katika eneo hilo hofu ya kuongezekana kwa magonjwa ya zinaa kama HIV hasa Kwa Vijana wa kike kutokana na kutumia Sehemu hiyo kama eneo la kuuuza miili Yao.
Wanasema siku za hivi karibuni wameshuhudia wasichana wadogo kuanzia umri wa miaka 15_20 wakisimama pembezoni mwa barabara na kufanya vitendo hivyo jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao hivyo serikali iangalie namna ya kutatua changamoto hilo.
“unakuta wasichana tena wadogo kabisa wamesimama kwenye malori pembezoni ya barabara wakifanya biashara haramu ya kuuza miili (dada poa) huku wengine wakitumia kama.sehemu ya kujificha hasa wahalifu hii ni hatari kwa taifa”alisema Mponzi Mwinyimvua mkazi wa mikumi
Mkuu wa mkoa Morgoro Adam Malima akiwa ameambata na kamati ya usalama mkoa wanafika katika eneo hilo ambapo anatoa maagizo kwa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa kuangalia namna ya kuweza kuthibiti hali hiyo ikiwemo kutafuta Sehemu maalum ya maegesho.
Anasema licha ya kuwa jambo hilo ni hatari kwa usalama wa wakazi wa eneo hilo lakini pia imekua ikichagia kutokea kwa ajali na ukosefu wa mapato hivyo upatikaji wa Kituo maalum cha maegesho ni mwarobaini wa changamoto hizo.