Zoezi la kuwaondoa wanajeshi wa Ufaransa Niger lililotangazwa na Emmanuel Macron mnamo Septemba 24 linaanza Alhamisi hii, Oktoba 5. Kwa mujibu wa jeshi la Ufaransa, muda unahesabilika kwani zozi la kuwaondoa wanajeshi 1,500 wa Ufaransa linapaswa kukamilika ifikapo mwisho wa mwaka wa 2023.
Kundi la kwanza la wanajeshi 400 wa Ufaransa waliotumwa Ouallam, kwenye mpaka wa Malo na Nigeria, ndio ambao wameondoka. Wanajeshi hawa walishiriki katika Operesheni Almahaou na wanajeshi wa Niger, ili kutoa ulinzi wa Liptako, nchini Niger.
Waajrshi hao ambao wamepangwa katika makundi mawili, huko Ouallam na Tabaré Baré, watasafiri magari yao hadi mji mkuu Niamey na kisha kuandaa safari yao kuelekea nchini Ufarasa.
Wataweka magari yao ya kivita katika utaratibu na kufafanua barabara ambayo itabidi kulindwa ili kufikia mji mkuu wa Niger. Umbali sio mrefu sana – karibu kilomita mia kadhaa- lakini kutokana na hali ya barabara, safari inaweza kuchukua siku mbili.
Mara baada ya kuwasili katika kambi ya kikosi cha wanaanga mjini Niamey, wanajeshi hawa 400 wataanza safari yao kwa ndege hadi nchini Ufaransa.
“Katika suala la udereva, tutafanya kile kilichopangwa.
Tutapanga jinsi ya kuondoka kwa utaratibu mzuri, kwa usalama na kwa uratibu na mamlaka za ndani,” wamebaini maafisa wakuu.