Michezo

PICHA: Emmanuel Okwi kakabidhiwa jezi yake Uganda

on

Najua zilikuepo stori nyingi za Okwi kurudi Tanzania juzijuzi baada ya kuvunja mkataba kwenye club yake ya majuu ikidaiwa ni kutokana na kutopata nafasi ya kucheza na baadae zikatoka taarifa kwamba kajiunga na club yake ya zamani ya Uganda.

Ni kweli, taarifa nilizonazo kutoka Uganda ni kwamba Emmanuel Okwi ni miongoni mwa Wachezaji wapya 6 wa Sports Club Villa ya Uganda waliotambulishwa leo ikiwa ni round ya pili ya ligi kuu ya Uganda iitwayo Azam Uganda Premier league.

Rais wa SC Villa Emmanuel Missaga amesema lengo lao kubwa ni kushinda ligi msimu huu pamoja na kwamba anajua wamefanya vizuri round iliyopita lakini round hii anaamini na hawa Wachezaji wapya watafanya vizuri zaidi.

Habai kutoka Uganda zinasema Emmanuel Okwi aliyevunja mkataba na club ya Sweden juzi kati amerejea Uganda na amesaini mkataba wa muda mfupi kumalizia ligi ya Uganda.

ALL GOALS: Yanga SC vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

ALL GOALS: Majimaji FC vs Simba SC Feb 4 2017, FULL TIME 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments