Mix

Tukio jingine la kigaidi lililoitisha Kenya leo kwenye parking ya magari.

on

NAKUMATT JUNCTION NAIROBIBaada ya tukio la Westgate ambalo lilichukua maisha ya watu wengi, jiji la Nairobi limekumbwa na tishio jingine la aina hiyo kwenye eneo la biashara la Nakumatt Junction Barabara ya Ngong ambapo yamekutwa masanduku manne ya kubebea risasi kwenye eneo la kuegesha magari kwenye vyumba vya chini (Basement).

Masanduku hayo yalipatikana ndani ya toroli la kubebea mzigo kutoka kwenye duka la jumla la Nakumatt ambapo walioshuhudia wamesema sanduku hizo zilikuwa zimeandikwa ‘explosion’ na walipoitwa wataalam wa mabomu  wakagundua kuwa sanduku ni za kubebea milimita 9 risasi za bunduki aina ya ceska ama Mp5 machine gun.

Masanduku hayo yaligundulika wakati wafanyakazi wakirudisha matoroli hayo ndani baada ya wateja kuyatumia na kuyaacha eneo la parking.

Tupia Comments