Mix

Idadi ya wanajeshi wa Uganda waliouawa na Al Shabaab kwenye mapigano Somalia…

on

Taarifa iliyonifikia ni kuhusu wanajeshi wa Uganda kuuawa na wapiganaji wa Al Shabaab, Somalia wakiwa kwenye kambi ya wanajeshi wa Muungano wa Afrika AU.

Miili ya wanajeshi 12 inatarajiwa kusafirishwa wakati wowote kwenda Uganda kwa ajili ya maziko ya Kitaifa.

Wanajeshi wa Uganda ni miongoni mwa kikosi cha wanajeshi 22,000 cha AU, kinachokabiliana na wapiganaji hao kutoka Somalia.

milita

Mmoja wa wanajeshi wa AU akiwa kazini

Ripoti nyingine zinasema wanajeshi waliouawa kwenye uvamizi huo katika kambi ya Janale, kilomita 90 kutoka Kusini Magharibi mwa mji mkuu Mogadishu, ni kati ya 20 hadi 50.

Wakazi wa eneo lililotokea shambulizi hilo zinasema shambulio hilo lilianza kwa shambulio la kujitoa mhanga lililotekelezwa kwa kulipua gari lililotegwa bomu kwenye lango la kambi hiyo, na kisha kukawa na ufyatulianaji wa risasi uliodumu zaidi ya saa moja.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments