Duniani

Watu wenye sura mbaya wamefunikwa na huyu Zimbabwe, kabeba na dola zake 500 za ushindi.. (+Video)

on

Kama vile ambavyo kuna mashindano ya watu wenye sura nzuri, mvuto, warembo, na mashindano mengine yote tuliyozoea, kuna mashindano ya wenye sura mbaya pia toka Zimbabwe.

Jamaa anaitwa Maison Sere, hana kibarua chochote rasmi kinachomuweka mjini lakini kagusa kwenye stage inayohusu mashindano ya watu wenye sura mbaya na kaibuka na ushindi wa dola 500 mkononi kama utani yani !!

2EA9B3F100000578-0-The_contest_attracted_35_participants_with_organisers_saying_the-a-11_1448124566984

Washiriki wengine wa shindano hilo wakiwa kwenye stage.

Unaambiwa kwenye mashindano hayo, William Masvinu ni jamaa ambaye amewahi kushinda Taji hilo mara tatu mfululizo amelalamika kwamba kumefanyika upendeleo ndio maana safari hii amelikosa taji hilo na kujikuta akishika nafasi ya pili, anachoamini ni kwamba kwa ubaya wa sura yake anastahili #1.

Maison-Sere

Maison Sere kwenye pozi lake.

Maison Sere hana meno kadhaa mdomoni, na amefanikiwa kuibuka na ushindi huo kwa kuwashinda washiriki wengine watano huku akijikunjia na mkwanja wake dola 500 ambazo ukizichenji zinagusa kama Milioni 1 hivi !!

Stori yake imegusa vichwa vya habari vya Kimataifa pia, unaweza kucheki ripoti yake kutoka kituo cha TV ya China CCTV.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments