Top Stories

Ugomvi kwa mganga mmoja afariki

on

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 65 Muthui Mwenga amefariki Dunia nchini Kenya baada ya kutokea ugomvi kati yake na Mganga wa Kienyeji mwenye umri wa miaka 80 katika eneo la Mathuki, Kaunti ya Kitui.

DCI wa Kenya amesema Muthui alikwenda kwa Mganga huyo kama Mteja na baadaye ugomvi ambao chanzo chake hakijajulikana ukaibuka na kupelekea majirani wa eneo hilo kuingilia kati baada ya kusikia makelele.

“Majirani walipofika walikuta Mganga ameumizwa kichwani na kwakuwa Watu wa eneo hilo wanamuheshimu sana Mganga huyo wakapata hasira na kumshambulia Muthui na akafariki papohapo baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani”

“C.E.O BARBARA AMEFANYA VURUGU LEO AKIINGIA VVIP, WALIKUJA NA TICKET ZA WATU WENGINE” – TFF

Soma na hizi

Tupia Comments