AyoTV

Ugomvi Trafiki na Madereva: Kamanda Mwakyoma afunguka”Mahusiano mabovu” (+VIDEO)

on

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam, Marison Mwakyoma amesema kilio kilichopo kwa sasa baina ya Maofisa wa Usalama barabarani ‘Trafiki’ na Madereva ni mahusiano mabovu.

Kamanda Mwakyoma amesema uhusiano umekuwa mbaya ambapo vitu vingi vinatendeka baina ya Madereva ama Askari, huku kila mmoja akijaribu kutetea upande wake.

“Ukiangalia dereava anapigana na askari kisha mwingine anachukua anaweka katika mtandao, sijajua kama kiwango hiki tulichofikia ni kizuri ?” amehoji.

Kutokana na hatua hiyo, amesema kinachofanywa na Jeshi la Polisi kwa sasa ni kujenga mahusiano mazuri baina ya Madereva na Askari ili kuhakikisjha hatua sahihi zinachukukiliwa badala ya watu kulalamika.

KATIBU WA CCM ASWEKWA NDANI, SABAYA APIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA CCM NA CHADEMA

Soma na hizi

Tupia Comments