June 19 2016, Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia na watoto ilitoa taarifa kuhusu kuwepo kwa ugonjwa usiofahamika katika wilaya za Chemba na Kondoa, mkoani Dodoma ambapo wakati huo kulikuwa na jumla ya wagonjwa 21 na vifo 7.
Leo June 25 2016 Waziri Ummy Mwalimu ametoa taarifa kwamba idadi ya wagonjwa imefikia 32 na idadi ya vifo imebakia 7 hii ni baada ya kuongezeka kwa wagonjwa 11 katika kipindi cha wiki moja.
Waziri Mwalimu amesema Wizara ifanya jitihda mbalimbali za kutambua kiini cha ugonjwa huo baada ya kupeleka jopo la wataalamu ili kufanya uchunguzi wa kina pia ameeleza kuhusu sampuli zilizofanyiwa utafiti…….
>>>’Sampuli mbalimbali zikiwemo, haja ndogo, haja kubwa, vinyama vya ini na sampuli za vyakula zilipelekwa katika maabara za mkemia mkuu wa serikali, maabara ya mamlaka ya chakula na dawa ‘TFDA’
>>>’Hadi sasa sampuli za nafaka pekee, zilizofanyiwa uchunguzi katika maabara ya TFDA ndio zilizoonyesha kuwepo kwa uchafuzi wa sumukavu ‘Aflatoxin’ katika sampuli za nafaka hizo’:- Waziri Mwalimu
Waziri ameongeza pia kuna uwezekano mkubwa kwamba ugonjwa huo umesababishwa na ulaji wa chakula kilichokuwa na sumukuvu na kuleta madhara.
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA JUNE 25 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB INSTAGRAM YOUTUBE