Rais William Ruto ameuthibitishia ulimwengu kwamba maambukizi ya virusi vya UKIMWI nchini bado ni kero kubwa haswa kwa makundi ya wanawake na vijana wa umri wa balehe.
Akizungumza Jumanne wakati wa mkutano wa ngazi ya juu kuhusu “Multilateralism Works: Uongozi na Kudumisha Makabiliano dhidi ya UKIMWI kufikia 2030 na Zaidi” huko New York, Ruto alifichua kwamba Kenya sasa inakaribia kufikia udhibiti wa janga, baada ya kufikia malengo ya kimataifa ya 95-95-95.
Hata hivyo, rais alifichua kwamba janga la UKIMWI bado ni changamoto kubwa kwa kina mama, wasichana na vijana wa balehe kutokaka na kile alisema ni kutokuwepo kwa usawa wa ufikiaji wa matibabu nchini.
“Janga hili linaendelea kuathiri vibaya vikundi vilivyo hatarini, pamoja na wanawake, wasichana, vijana wa balehe, na idadi kubwa ya watu, ikichochewa na ukosefu wa usawa wa kiafya, unyanyapaa na ubaguzi,” rais alisema