Michezo

Kapombe kapinga taarifa iliyotolewa dhidi yake

on

Beki wa Simba SC na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Shomari Kapombe amekanusha taarifa zilizoripotiwa kuwa ameumia tena, wakati huu akiwa kambini na timu ya taifa ya Tanzania kujiandaa na michuano ya AFCON 2019 itakayofanyika nchini Misri.

Kapombe amekanusha kuwa taarifa hizo sio za kweli kupitia ukurasa wake rasmi wa instagram “Ni jambo la kusikitisha na linaloumiza kwa kias kikubw kwa taarif hii inayoendelea kusambazwa na vyomb vya habari na watu mbalimbali kuwa nimeumia /nimejitonesha jerah langu hakika hz habari sio za kweli kabisa na hazina uhakika na ukweli wowote”

“katika siku niliyoumia ni leo najiuliza nitaumiaje nikiwa nipo nyumb na camp sijaingia au kufanya mazoez na timu ya taifa??? mm niko mzima na nafanya mazoezi yang vzr nafuata program yng niliyoachiwa na fitness coach wangu wa Simba”

“Mimi pamajo na familia yangu tumeumizwa na taarifa hii ni kubwa na nzito kwet naomba vyombo vya habari kutoa taarifa iliyokuwa sahih na yenye ukweli wa asilimia mia. Wanasimba na watanzania wote, wapenda soka napenda kuwaambia kuwa mimi niko sawa na hakuna ukweli wwt kuhus mimi kuumia tena hz taarifa sio sahihi kwa wote waliyotoa taarifa hz au kusambaza….Mungu nipe uvumilivu na haya yatapita”

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments