Michezo

Ed Woodward anajitoa kwenye lawama za Man United

on

Makamu mwenyekiti wa Man United Ed Woodward amejitoa kwenye lawama kuhusiana na suala ambalo limekuwa likiendelea kwa siku za hivi karibuni, kuhusiana na usajili wa wachezaji wa timu hiyo hususani baadhi ya watu wakimtupia lawama kwa kudai kuwa hatoi pesa za usajili kwa wachezaji sahihi.

Ed Woodward ameeleza kuwa sehemu pekee ambayo huwa anahusika katika ununuzi wa wachezaji ni kusaini pesa tu za malipo na sio vinginevyo, tofauti na mashabiki wanavyoamini kuwa ana nguvu ya kumsajili au kuwasajili wachezaji mbalimbali.

Ed Wood

“Maamuzi kuhusiana na kusajili wachezaji na kuinua vipaji yanafanywa na wataalam wa soka, mimi nahusika kusaini pesa tu, kocha ana kura ya kumchagua mchezaji anayemtaka hatuwezi kumsajili mchezaji ambaye kocha hamtaki kwa sababu hatompanga pili idara ya kusaka vipaji ndio wana kura pia ya kumchagua mchezaji”>>>Ed Woodward

“Mimi sihusiki kwa hilo kama watu wanavyofikiria, kuna fikra ipo kwamba nakaa naangalia YouTube nachagua wachezaji mimi sichagui, kuwa na jicho la kujua uwezo wa mchezaji ni sanaa, sina uwezo wa nia ya kufanya hivyo”>>> Ed Woodward

AUDIO: SERGIO AGUERO WA MAN CITY AMEPATA AJALI

Soma na hizi

Tupia Comments