Mix

Uhamiaji wamekuja na hii ripoti ya operesheni ondoa uhamiaji haramu

on

Idara ya Uhamiaji imekuwa ikiendesha Operesheni ondoa uhamiaji haramu tangu mwezi Desemba mwaka jana katika operesheni hiyo iliyoonyesha mafanikio ambapo takribani raia 4792 wa kigeni wamekamatwa kwa kukiuka sheria, kanuni na taratibu za uhamiaji katika kipindi cha January hadi april mwaka huu.

Akizungumza mbele ya wanahabari  Kaimu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji Abass Irovya amesema operesheni hiyo imefanikiwa ambapo raia 1796  wamefukuzwa nchini kwa kukiuka sheria za uhamiaji……….

>>>“Wananchi walio wengi wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa Idara yetu kutokana na uelewa wao kuongezeka kwa sababu tunayo programu ya kutoa elimu kwa umma na imeonyesha mafanikio makubwa”

Irovya aliongeza kuwa waliohukumiwa kifungo ni raia 132 na 383 kesi zao zinaendelea kwenye mahakama katika Mikoa mbalimbali hapa nchini.

Raia 388 walilipa faini hali iliyochangia kuongeza mapato ya Serikali kutokana na kukiuka sheria na Kanuni za uhamiaji hapa nchini. Kwa upande mwingine kesi 509 zinaendelea katika mahakama mbalimbali hapa nchini na raia 294 waliachiwa huru kutokana na mahakama kutowatia hatiani.

Idara ya Uhamiaji ina Vituo takribani 60 katika Mikoa Mbalimbali hapa nchini baadhi vikiwa katika Mikoa ya Tanga, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Katavi, Kigoma, Simiyu ambapo Idara hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu athari za raia wa kigeni wanaoingia nchini bila kufuata sheria na taratibu za Uhamiaji.

ULIIKOSA HII STORI ZA MWANAUME KUWAINGILIA KISIRI WANAWAKE KIGOMA, MASHUHUDA WALIVYOELEZA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments