Habari za Mastaa

Alichoshuhudia Madee baada ya wezi kwenye bodaboda kupora pochi barabarani.. (Audio)

on

Madee

Kwenye show ya PowerBreakfast August 05 2015, Madee kasikika akiwa na Soudy Brown.. U Heard imesikika hapahapa na ishu ni wizi ambao Madee kaushuhudia maeneo ya Sinza Dar usiku.

Dada mmoja kanyang’anywa pochi yake na jamaa wawili waliokuwa kwenye Bodaboda, mbele kidogo wakayumba wakaanguka.. watu wakawakimbiza mpaka kuwakamata.

Madee anasema pikipiki ya hao jamaa ikachomwa moto na wakaanza kupigwa, mmoja alifanikiwa kukimbia akajificha kwenye mtaro wa maji, Polisi wakamtoa wakaondoka nae lakini mmoja alipigwa mpaka akafa hapohapo.

Sauti ya U Heard iko hapa, msikilize Soudy Brown na Madee sasa kwenye hiyo story ilivyokuwa.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments