Habari za Mastaa

Ommy Dimpoz alitoa machozi jukwaani, kisa nini? Soudy Brown alimuona pia..

on

 DSC_6352

Weekend iliyopita Escape One kulifanyika show iliyowakutanisha mastar wakubwa ndani na nje ya TZ kama Christian Bella, Ruby, Ali Kiba, Kassim Mganga, Ommy Dimpoz, Msami, na Alicious kutoka Kenya, WOTE kwenye stage moja.

Moja ya hits ambazo zimependwa SANA ni ‘Nani Kama Mama‘- collabo ya Ommy Dimpoz na Christian Bella.

Soudy Brown alikuwa mmoja ya watu waliokuwa kwenye show hiyo Escape 1, akamuona Ommy akitokwa machozi wakati wanaimba wimbo huo kwenye stage.. Ommy akashindwa kuendelea akashuka, Soudy akamfuata kujua tatizo ni nini?

Dimpoz  amesema aliandika wimbo huo kwa sababu ya kumbukumbu ya kifo cha mama yake aliyefariki miaka 15 iliyopita, alimuacha akiwa mdogo sana.. wakati anaimba wimbo huo alikumbuka mapenzi ya mama akatamani kama mama yake angekuwepo.. ni hicho tu kilichomtoa machozi.

Bonyeza play hapa chini kusikiliza stori yote…


Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>>  Twitter Insta FB  na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments