Habari za Mastaa

Mwanamuziki wa Bendi kamvua hereni na cheni mpenzi wa zamani, kisa chenyewe nini?

on

You-heard1

Soudy Brown akiwa kwenye mizunguko yake akakutana na tukio alipofatilia akaambiwa kuwa kuna msanii mmoja wa dance amempora mpenzi wake wa zamani vitu mbalimbali vya thamani ikiwemo hereni, mkufu na pochi.

Mwanamke aliyeporwa amesema alikuwa na uhusiano na msanii  huyo lakini wameshaachana na alishamueleza kuwa hamhitaji tena, ila walipokutana alimuambia kuwa popote atakapomkuta lazima amfanyie fujo ndipo.. mwanamke huyo amesema mwanamuziki huyo amemvamia rafiki yake akamnyang’anya pochi na kumvua hereni na cheni.

Christian Bella ambae alikuwa akifanya show eneo hilo amesema alisikia watu wakigombana lakini hakufatilia kujua nini kinaendelea, alihofia kupigwa ngumi.

Bonyeza play hapa uisikie stori yote ya U Heard

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter,Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>>  Twitter Insta FB  na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa>>>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments