Habari za Mastaa

G Nako amepoteza mil.6 kwenye kikao cha wasanii !! Ishu yenyewe ilikuwa hivi.. (+Audio)

on

Kwenye U Heard January 7 2016 Soudy Brown ana stori ya kusikitisha kidogo leo !!

G Nako mkali wa chorus kutoka crew ya Weusi kwa bahati mbaya kapoteza pesa ambayo ni dola 3,000 wakiwa kwenye kikao cha wasanii !!

Kapatikana Baba Levo, ambaye amesimulia kwamba mazingira yanaonesha G Nako alikaa akiwa amezungukwa na watu wake wa karibu ambao sio rahisi kumwibia G Nako, kwa hiyo huenda pesa hiyo kaangusha.

Nikk wa Pili ambae ni msemaji wa Weusi amesema bado hawajajua ni mazingira yapi pesa hizo zimepotea lakini zilikuwa ni dola 3,000 ambazo ni zaidi ya milioni 6.5 kwa pesa ya Kitanzania.

Pole sana kwa mtu wetu G Nako.. U Heard hii hapa, Soudy Brown akiongea na Baba Levo pamoja na Nikk wa Pili.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments