Habari za Mastaa

Shetta yuko kwenye show Mwanza, nini kilifuatia baada ya vurugu kutokea?? >> #UHeardD (Audio)

on

Shetta TZA

Mkali wa hit ya ‘Shikorobo’, baba Qaira aka Shetta alikuwa kwenye show Mwanza… mtu kamsaka Soudy Brown na kumpa story kwamba ilitokea vurugu baada ya show hiyo kuisha, Shetta kamuahidi mtu zawadi na hakumpa zawadi hiyo.

Soudy akamcheki Shetta.. Shetta amesema ni kweli yuko Mwanza ambako alikuwa anafanya show, kulitokea vurugu ambazo watu walizuia gari yake isiondoke eti jamaa aendelee na show.. Shetta amesema kuna mtu alipiga risasi hewani ili watu watawanyike gari iondoke, ila hakuna mlinzi wake aliyepiga risasi.

Ishu ya zawadi Shetta amesema sio kweli, yeye kama akiahidi kutoa zawadi huwa inatoka hapohapo kwenye stage.

255 iko kwenye hii sauti hapa, huyo jamaa wa Mwanza na Shetta wote wamesikika hapa.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments