Habari za Mastaa

TANESCo walivyokatisha nyumbani kwa Wema Sepetu, kilichofatia ni hiki hapa.. na Idris yumo ?? (+Audio)

on

Oparesheni ya TANESCO kukagua nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa imeendelea kama ambavyo kumekuwa na story kwenye vyombo vya habari !!

Story imegusa mitandaoni, ikamfikia Soudy Brown… leo akaanza na kiongozi wa TANESCO, jamaa amesema walifika wakagundua kuna tatizo kwenye mfumo wa mita ya LUKU nyumbani kwa Wema, walipohitaji maelezo ya wanaoishi kwenye nyumba hiyo, Wema hakuwepo na badala yake akatokea Idris.

Soudy Brown akageuka kumcheki IdrisIdris amesema alikuwa anapita kwenda kwenye mishemishe zake ndio akakutana na ishu hiyo ya TANESCO nyumbani kwa Wema, ila hajui chochote kinachoendelea kwa sababu haishi na Wema kwenye nyumba hiyo.

U Heard hii hapa kwenye sauti yote mtu wangu.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments