Habari za Mastaa

Mengine yameibuka ya Range Rover ya Wema Sepetu, hapa yamemfikia Soudy Brown.. U Heard (+Audio)

on

Moja ya stori exclusive kabisa ambazo niliwahi kuzisogeza hapahapa kwenye millardayo.com ilikuwa interview ya Martin Kadinda kuhusu gari ya Wema Sepetu.. kwenye majibu ya Martin alisema gari ya Wema yuko nayo kihalali, hakuna deni lolote la kodi alikwepa kwenye kulipia gari hilo aina ya Range Rover aliyojipa zawadi.

WEMA

Soudy Brown kayanasa mengine, amesema kulikuwa na stori kwamba kuna watu walikamata garni hiyo ikiwa haina baadhi ya nyaraka zake, mambo yakaenda baadae jamaa wakalikamata gari hilo na kuondoka nalo.. Soudy akamcheki Martin Kadinda, jibu lake ni kwamba na yeye aliisikia story ya namna hiyo lakini hakuwa anajua kinachoendelea.

MARTIN

Martin amesema alimtafuta Wema, akaenda nyumbani kwake na kukuta gari hilo lipo, alipomuuliza Wema kuhusu stori ya gari kukamatwa amesema Wema alimwambia hakuna sababu ya kuuliza gari wakati analiona lipo kwake halijakamatwa.

Hayo ndio ya Soudy Brown kwa leo, U Heard yote one to one na Martin Kadinda na stori yote ya gari hii hapa kwenye sauti zao mtu wangu.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments