Habari za Mastaa

Ni kweli Edo Boy kampeleka Polisi Young Killer kisa deni? Stori ipo kwa Soudy Brown…#UhearD

on

MSODOKI

Kama kawaida ya Soudy Brown leo kazipata nyepesi kuhusu msanii Edo Boy kampeleka polisi mwenzake Young Killer, kisa inasemekana wanadaiana pesa..

Shuhuda wa tukio hili alimwambia Soudy kuwa Young Killer alishindwa kumlipa mwenzake hela yake na wakakunjama mbele za watu wakitaka kupigana huku wakielekea Polisi.

Edo Boy ameomba hayo mambo yaishe na hataki kuyazungumzia, amesema hajui Young Killer alipo kwa sasa…amesema hayo ni mambo private haina haja ya kuyaweka hadharami.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments