Habari za Mastaa

Rapper AKA aligoma kufanya kazi na Joh Makini? Utapeli wa Mdundo.com je? kasikika pia Fella kuhusu albam mpya..#255 (Audio)

on

news burdn

Mwishoni mwa wiki iliyopita CCM ilimtangaza Dk.John Magufuli kuwa mgombea Urais kupitia chama hicho huku na yeye akimchagua Makamu Mwenyekiti wa bunge la Katiba Samia Suluhu kuwa mgombea mwenza..

XXL ilimteua Joh Makini  kuyfanya collabo na Rapper AKA wa Afrika Kusini..anasema kama angekuwa hana ngoma alizorekodi ingekuwa vigumu kufanya kazi na msanii huyo kutokana na kuwa na mambo mengi, baada ya kumshirikisha baadhi ya nyimbo zake alikubali na ikawa kazi rahisi kwani alizipenda sana nyimbo zake ikiwemo ngoma ya ‘Nusunusu’.

Nick Mbishi amewalaumu Mdundo.com kwa kuwazungusha kuhusu maslahi..wamekuwa na sababu zisizo na maana na kuamua kufanya utapeli.

Amesema wasanii waliofaidika na kupataa pesa nyingi kupitia Mdongo ni Songa,Jux, Barakah Da Prince na wengine…lakini wengine hawajapata pesa zao mpaka sasa.

Said Fella alitangaza kurudisha albamu za wasanii..amesema kuanzia mwezi wa sita zingeanza kutoka lakini mpaka sasa bado..amesema sababu ni VAT ya 18% wanataka ilipwe na msanii jambo ambalo haliwezekani ni bora kugawana nusu kwa nusu.

Wasikilize hapa…

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments